UWAKILI

UTANGULIZI
Luka 12:42 - 44 inasema: "… Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote"

Kanisa leo liko katika hali ya uhitaji na umaskini kwa sababu halijagundua kwamba siri ya kuondokana na hayo (uhitaji na umaskini) ni kwa mtu kuwa wakili mwaminifu.

Mtu anaweza kujiuliza kuna uhusiano gain baina ya uhitaji na umaskini kwa upande mmoja na kutokuwa wakili mwaminifu kwa upande mwingine. Kwa mtu anayejiuliza swali hilo, ningependa kumpa jibu kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya mambo hayo. Ukitaka kuondokana na uhitaji na umaskini basi jambo la kufanya ni kuwa wakili mwaminifu.

Nimeshangazwa kuona Wakristo wengi hapa Kanisani ambao hawatoi zaka. Wengine hata walikuwa wanatoa zaka lakini baadaye, sielewi kwa sababu zipi, wameaacha kufanya hivyo.

Wengine husema mahubiri ya namna hii ni mahubiri ya „kimwili" ambayo yamelenga „baraka za mwilini" na siyo za rohoni. Nataka niwajibu watu wa jinsi hiyo haraka sana kwamba Injili ya Yesu Kristo ni Injili iliyokamilika. Ina uwezo wa kuhudumia roho, nafsi na mwili wa mwanadamu. Si kweli kwamba Mungu anajishughulisha na roho ya mwanadamu tu pekee na kwamba hajali kuhusu mwili wa mwanadamu. Si ni Mungu aliyemwumbia mwanadamu mwili? Tuhibiripo mambo haya, twalihubiri Neno la Mungu pia.

UWAKILI
Mahali pa kuanzia ni kujiuliza uwakili ni nini, na wakili ni nani? Ninapenda kutoa ainisho ya neno „wakili" kuwa ni yule mtu ambaye amewekwa ili aangalie nyumba na shughuli za mtu mwingine.

Katika Agano Jipya, wakili alipaswa, kama wajibu wake, kumtolea bwana wake hesabu (ama maelezo kamili) juu ya jinsi alivyotimiza wajibu wake. Kutokana na hili, wakili sharti awe ni mtu aliye mwaminifu. Ndiyo maana, Bwana wetu Yesu Kristo, katika mistari ile ya Luka 12: 42 - 44 tuliyoisoma hapo juu, anauliza ni nani aliye wakili mwaminifu, ambaye bwana wake atamkuta akitimiza yale aliyoagizwa na bwana wake hapo bwana wake atakaporudi.

Wakristo ni mawakili wa Mungu, ambao Bwana Yesu amewaweka ili kuangalia mambo ya Mungu hapa duniani. Kwa hiyo basi, Wakristo tunawajibika kutoa hesabu (ama maelezo kamili) kwa mambo yote yale ambayo Mungu ametupa. Pia tunawajibika kutoa hesabu kuhusu wajibu wetu kwa Mungu wa kuihubiri Injili na kuliangalia Kanisa la Bwana. Wakili siyo mwenye mali. Anawajibika kwa mwenye mali.

Katika Luka 16: 1 - 2, twasoma:
„Tena, aliwaambia wanafunzi wake, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyekuwa na wakili wake: huyu alishitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake. Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena"

Na pia katika 1 Kor. 4: 2 imeandikwa:
„Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu"

Utaona jinsi gani uaminifu unavyohitajika katika mawakili. Mtu asipokuwa mwaminifu hawezi kuwa wakili.

    Mtu aweza pia kuangalia mistari ifuatayo kuhusiana na uwakili na uaminifu:
  • Lk. 12: 42
  • Mw. 1: 28 - 30
  • Kol. 1:25, na
  • 1 Pet. 4: 10.
MAENEO YA UWAKILI
Kuna maeneo ambayo Mungu ametupa kuwa mawakili kwayo na ambayo tunatakiwa kuwa waaminifu. Maeneo haya ni haya yafuatayo:
  1. Muda:
  2. Vipawa vyetu na karama
  3. Hazina zetu
Ni vyema tukayaangalia maeneo haya moja baada ya jingine:

1. Muda:
Muda ni mtaji ambao Mungu ametupa ili tuutumie vizuri. Nadiriki kusema katika mitaji yote ambayo mtu aweza kuifikiria, hakuna mtaji wa maana zaidi kuliko muda. Tofauti kati ya maskini na tajiri iko katika jinsi ambavyo kila mmoja wao anavyoutumia muda wake.

Kuna wengine ambao wanasema, „ Aaa, niko hapa bwana, napoteza muda!..." Muda ukisha potea haiwezekani kuupata tena. Hata ungalipanda chombo chenye uwezo wa kwenda kasi kuliko kasi ya nuru isafiripo, bado hutaweza kuupata muda uliokwisha potea. Ni vyema usipoteze muda.

Nadiriki kusema kwamba wakazi wan chi za Magharibi wamewashinda wakazi wa nchi zinazoitwa zinaendelea kwa jinsi ambavyo wanatumia muda wao kwa umakini na uuangalifu mno. Mke wangu, ambaye ni mtu kutoka katika nchi mojawapo ya magharibi, amenisaidia kuona umuhimu wa kuto[poteza muda. Kwa mfano, ameweka vijigazeti na vijitabu chooni ili hata muda ule ambao mtu anakuwa anajisaidia chooni aweze kuutumia kwa kusoma! Bila shaka pia umeona watu wengine ambao watumia muda wao wawapo katika basi ama mahali pengine pa kusubiri kwa manufaa, mfano kwa kusoma, hata kama ni katika daladala!

Biblia inatufundisha kuutumia muda wetu vyema. Zaburi 90: 12: "Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima"

Efeso 5: 15 - 16:
"Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima, bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu"

Wekeza ("invest") muda wako katika vitu na mambo ya maana, yadumuyo milele. Kuna mambo yasiyo dumu, na kuna mambo yadumuyo milele. Mimi nakushauri uwekeze muda wako katika mambo yadumuyo milele. Mifano ya mambo yadumuyo milele ni:
  • Neno la Mungu: Tumia muda wako kusoma na kujifunza Neno la Mungu.
  • Maombi: Tumia muda wako katika maombi
  • Kazi ya Mungu, kama vile ushudiajiaji n.k.
2. Vipawa vyetu na Karama
Vipaji tulivyopewa na Mungu

Mfano
Mwili, Ujuzi, Hekima nk.

"Usimwue farasi kabla hajafikisha ujumbe"

Usiuwe mwili wako kabla hujafikisha ujumbe {Injili}

Pata muda wa kupumzika

Fanya mazoezi N.k
Nafasi tulizonazo katika jamii
Tumia nafasi uliyo nayo kwa hekima

Ester alitumia nafasi aliyo kuwa nayo kuwaokoa Israel pia Yusufu alitumia nafasi aliyo kuwa nayo katika jamii kuwasaidi ndugu zake ambao walikuwa hawana chakula

Karama za kiroho -1korinto 12: 4 -7

3 Hazina zetu:
Uwe maskini uwe Tajiri unaitaji kuelewa kanuni za Baraka zifuatazo:-
a} Kanuni ya kurejeshewa Luka 6:38 Mithali 11:24-31
{Zaburi 41:1-3} 2Wakorinto 9:6 Mithali 19:17

b} Kanui ya kulinganisha kiwango na kipato: - Luka 21:1-4

Kanuni ya kutoa kwa moyo wa furaha. 2 kor 9:7

Kanuni ya baraka toka juu 2 kor 8 - 11

Kanuni ya kupokea toka kwa wengine toka kwa wengine pale unapokuwa mhitaji. 2 kor 8 - 15.

Fedha.
Kuna kanuni za kimungu za kukufanya uwe wakili mwaminifu kwa habari ya fedha.
  1. Uitunze na kuijali familia yako 1 Tim 5:8 Lakini mtu yeyote asiyewatunza.........
  2. Usiwe mpenda fedha 1 Tim 6:10
  3. Toa kwa kadri ya ulivyonavyo. 2 kor 8:12
  4. Utoaji wako utokane na kuongozwa na Roho Mtakatifu na pia na misingi ya ki-biblia 2 kor 9:7
  5. Uwe mkarimu Hebr 13:16, 1 Yoh 3:17, 1 Tim 6: 17- 19, Mhu 11 : 1 - 2.
KIKUMI (ZAKA)
Bwana anaagiza tutoe zaka (kikumi) Lawi 27:30-33 , malimbuko (Mithali 3:9) kumb 14:22

Katika Agano jipya, Bwana Yeu aliagiza Luka 11:42, Math 23:23

Kanuni ya kikumi
10% ya mapato yako kabla ya makato.

Kikumi katika agano la kale kilitumika Kuwatunza maskini na wahitaji katika israel Kutoka 23:11 Kuwatunza walawi Kumb. 18 1 - 5

Agano Jipya Kuwaatunza maskini Mdo 4 : 34 - 37 Rum 15:26-27
Kuwatunza wahubiri na waalimu Galatia 6:6 1 Kor 9:14 Waf 4:15-18 Luka10:7

Mambo ya kukumbuka.
Sisi ndio tunaoamua tubarikiwe kiasi gani Luka 6:38 Mal3:7-10 Mdo 20:35

Unachopanda ndicho unachovuna Galatia 6:7

Kutumia mali zetu kwa ajili ya Mungu ni kuwekeza Luka 12:33

Mungu ndiye akupaye nguvu za kutajirika Kumb 8:18

Mungu ndiye mwenye mali zote na vitu vyote ni vyake Zab 24:1

HITIMISHO.
Hab 3:2 Labda unamwitaji Mungu afufue utoaji uliolufa katika Maisha yako. Mungu ni Mwingi wa rehema.
1. Vipawa vyetu na karama:
2. Hazina zetu:
MUNGU AKUBARIKI



Na Mch.
Lusekelo Mwaipyana


All Content © 2003
Gospel Power Center
Muta + Uswege Designs